Petit Man amvaa Shilole

Enjoy Your Life
Baada ya Nuh Mziwanda kuachia video ya Jike-Shupa inayomuonesha msichana anayefanana na Shilole (aliyekuwa X girlfriend wa Nuh) hali hiyo imezua gumzo mitaani.

Nuh Mziwanda alipohojiwa na Friday Night Live alisema kuwa wazo la video hiyo lilitolewa na Director ambaye ni Msafiri wa Kwetu Studios. Lakini eNewz ilichimbua na kupata stori kuwa Petit Man ndiye aliyeandaa wazo hilo la video na kumtafuta mdada aliyefanana na Shilole.

Alipopiga stori na eNews Petit Man na alikanusha kuwa hakudhamiria kumkejeli Shilole bali nia yake ilikuwa ni kutengeneza wazo linaloendena kabisa na nyimbo hiyo. Lakini kuhusu mdada huyo kufanana na Shilole mpaka Tattoo alizojichora Petit hakusema chochote.

Na kuhusu gari anayotumia Nuh Mziwanda kusemekana kuwa ni gari ambayo bado ipo kwenye biashara inauzwa, Petit akafichua siri kuwa yeye ni mfanyabiashara wa magari, lakini gari hiyo ya Nuh ni mali ya Nuh na haiko kwenye mnada kama inavyosemekana.

Subscribe to update the latest articles via email:

Add A Comment Below